Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila ametoa sababu za kwa nini mkoa huo hauendelei kwa haraka kibiashara akitaja sababu mojawapo ni wakazi wake wengi kuchelewa kufungua biashara asubuhi.
Pia, amesema wakazi wa mkoa huo wengi wanapenda kubishana na kutumia Kingereza ‘kingii’ hivyo amesema hataki Kingereza anachotaka ni namna gani wakazi hao wataweza kutumia elimu waliyonayo ili kuleta maendeleo.
Chalamila ametoa kauli hiyo mjini Bukoba katika mkutano wa ndani wa wanachama wa CCM uliohutubiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Abdulrahman Kinana.
Ещё видео!