Mapigo ya Moyo kwenda katika kipindi cha Ujauzito ni hali ya kawaida,Tafiti zinaonesha kwamba 60% na zaidi ya Wajawazito hupata Dalili hii ktk kipindi chote cha Ujauzito.
Kwa kawaida Mapigo ya Moyo huwa ni Mapigo 70 kwa dakika 1, Lakini Mjamzito huweza kuwa na mapigo 90 hadi 100 kwa Dakika 1.
Mapigo ya Moyo huanza kwenda mbio Mimba inapofikisha Wiki 12 hadi Wiki 16 lakini pia Mapigo Moyo huongezeka zaidi Mimba inapofikisha wiki 32 hadi 36 ambapo huongezeka kwa asilimia 30 hadi 50.
Mapigo ya Moyo kuongezeka ktk kipindi cha Ujauzito huweza kuwa ni hali ya kawaida au huashiria Ugonjwa fulani, hivyo Mjamzito anatakiwa kuchukua tahadhari ili kuondokana na athari ambazo zinaweza kutokea kwa Mtoto na Mjamzito wenyewe.
Mambo yanayopelekea Mapigo ya Moyo kwenda mbio katika kipindi cha Ujauzito yamegawanyika katika sehemu kuu mbili;
1. Mabadiliko ya kawaida katika kipindi cha Ujauzito.
2. Magonjwa mbalimbali kwa Mjamzito.
KUNDI LA 1: Mambo yanayopelekea Mapigo ya moyo kwenda mbio kutokana na Mabadiliko ya kawaida ktk kipindi cha Ujauzito, Mambo hayo ni kama yafuatayo:
I. Ongezeko kubwa la Damu katika kipindi cha Ujauzito, Kwa kawaida kutokana na Ongezeko la uhitaji wa chakula na Hewa safi kwa Mtoto tumboni, Damu huongezeka kwa 40% hadi 50% ili kukidhi mahitaji.
II. Mabadiliko ya homoni, Ongezeko la homoni za Estrogen na Progesteroni , huweza kupelekea Mapigo ya moyo kwenda mbio.
III. Kuto kuwa Maji ya kutosha Mwilini mwa Mjamzito.
IV. Baadhi ya Vyakula vyenye Caffeine
Mfano ; Chai, Kahawa na Soda aina za Coca-Cola na Pepsi.
V. Msongo wa Mawazo na Uoga.
VI. Mazoezi au kutembea kwenye sehemu zenye miinuko kwa Mjamzito.
KUNDI LA 2; Huashiria Magonjwa fulani kwa Mjamzito Mfano;
I. Magonjwa ya Moyo.
II. Mishipa ya Damu ya Moyo kutopeleka Damu ya kutosha kwenye Moyo.
III. Ongezeko la Tezi ya Madini Joto.
IV. Presha katika Ujauzito.
V. Upungufu wa Damu kwa Mjamzito.
VI. Magonjwa ya Kisukari na nk.
UONAPO MAPIGO YA MOYO YANAKWENDA MBIO YANAAMBATANA NA DALILI ZIFUATAZO UNATAKIWA KWENDA HOSPITALI.
Dalili Kama;
I.Maumivu ya kifua.
II. Kupata kizungu zungu.
III.Kuanguka ghafla au Kupoteza Fahamu.
IV. Kutoa Jasho au Kukohoa Damu na nk
ENDAPO MAPIGO YA MOYO YANAKWENDA MBIO KUTOKANA NA MABADILIKO YA KAWAIDA KATIK UJAUZITO HUHITAJI DAWA UNAHITAJI KUZUIA HALI HIYO KWA KUFANYA MAMBO YAFUATAYO:
1. Kupunguza Msongo wa Mawazo au Uoga katika Ujauzito wako.
2. Kuepuka vinywaji vilivyo na Caffeine vilivyo tajwa hapo juu.
3. Kuepuka kunywa Pombe katika kipindi cha Ujauzito.
4. Kupata Muda wa kupumzika na kutulia.
5. Kunywa Maji yakutosha katikati kipindi cha Ujauzito.
6. Matumizi ya Dawa za kuongeza Damu katikati kipindi cha Ujauzito.
ENDAPO DALILI ZINAENDELEA KUWEPO UNAHITAJI KWENDA HOSPITALI KUFANYIWA VIPIMO
mfano;
1. ECG kwa ajili ya kuangalia Umeme katika Moyo.
2. X-ray kuangalia kama Moyo umetanuka.
3.Presha katika Ujauzito
4. Uwingi wa Damu katikati kipindi cha Ujauzito.
5. Homoni zitokanazo na Tezi ya Madini Joto na nk.
KUMBUKA:
Katika Wanawake Wajawazito wote wanaopata Dalili ya Mapigo ya Moyo kwenda Mbio, 5% hadi 12% hupata athari kubwa kiafya endapo walikuwa na dalili hiyo katika kipindi cha Ujauzito.
#MamaAfyaBora
#DrMwanyika
#MapigoYaMoyo
Ещё видео!