Meza ya Bwana ni moja ya Maagizo makuu ya Bwana wetu Yesu Kristo kwa kanisa, pamoja na Ubatizo wa maji mengi haya ni maagizo makuu pamoja na kuhubiri injili. Kutokana na maagizo haya moja ya mambo ambayo Yesu alituagiza tumkumbuke kwa mateso yake ni kwa njia ya kula mwili wake na kuinywa Damu yake kama kumbukumbu ya mateso yake.
Hakuna njia ya mkato ya kumkumbuka Yesu hakutuagiza kuweka sanamu au chochote mfano wa mbinguni bali kula na kunywa Damu na mwili wake tu, Fanyeni hivi kwa ukumbushio wangu……Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa,Kikombe akisema, kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo,kwa ukumbusho wangu. 1 Wakorintho 11:25
Meza ya Bwana hutambulika kwa majina kadhaa kama ilivyoelezwa kwenye maandiko Matakatifu.
• Meza ya Bwana (Lord’s Table)
• Ushirika Mtakatifu (Holy Communion)
• Chakula cha mwisho (Last Supper)
1.NINI MAANA YA MEZA YA BWANA?
Ni mojwapo ya agizo kuu la Bwana mwenyewe kwa mitume na Kanisa lake
Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa,akise
ma,Kikombe hiki ni Agano Jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo,kwa ukumbusho wangu. 1Wakortho 11:25
Lilianzishwa na Bwana mwenyewe kabla ya kifo chake Luka 22:14-20
Mathayo 26:26-29, Nao walipokuwa wakila,alitwaa mkate, akabariki, akaumega,akawapa,akase ma,Twaeni ;huu ndiyo mwili wangu…..Marko 14:22
2.KWANINI TUSHIRIKI MEZA YA BWANA?
• Kwanza tuna kumbuka kifo na mateso ya Kristo
Maana kila mlapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki,mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo, 1Wakorintho 11:26
• Tafsiri tofauti juu ya ushirika wa Meza ya Bwana, Kuna wanaoamini ni kumbukumbu tu.
Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa,akise
ma,Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo,kwa ukumbusho wangu. 1 Wakorintho 11:25
Lakini kwa mtazamo wa kimaandiko ni zaidi ya kumbukumbu kwa mujibu wa maaelekezo ya Bwana Yesu Kristo alipokuwa anawafundisha wanafunzi wake. Basi Wayahudi walishindana wao kwa wao, Awezaje mtu huyukutupa sisi mwili wake ili tuule? Basi Yesu akawaambia,Amini amini, nawaamba ,Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake,hamna uzima ndani yenu.Yohana 6:52-53.
Kuna nguvu ya uzima ndani ya Damu ya Yesu Kristo, Uhai unaoingia ndani yetu
3.FAIDA ZA KUSHIRIKI MEZA YA BWANA
• Tunapata ushirika kamili na Kristo kupitia kikombe cha Damu yake na mkate ambao ni mwili wake.
Basi Yesu akawaambia,Amini amini, nawaamba ,Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake,hamna uzima ndani yenu.Yohana 6:53.
• Katika ushirika wa Meza ya Bwana tunapata uzima wa milele na tunakaa ndani ya agano la damu na mwiliwake
Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu ,nami hukaa ndani yake. Yohana 6:56
• Tunapata uhai na uzima katika miili yetu, Uponyaji na nguvu za ki-ungu kupitia Damu ya Yesu. Yohana 6:57-58, Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi,nami ni hai kwa Baba,kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi.Hiki ndicho chakula kishukacho kutoka mbinguni;si kama mababa walivyokula, wakafa;bali akilaye chakula hicho ataishi milele.
Ещё видео!