KISA CHA ISRA NA MIRAJ
Aya 1: Israi Maana Ametakasika aliyempeleka usiku mja wake kutoka Msikiti Mtakatifu mpaka msikiti wa mbali ambaotumevibariki vilivyo kandoni mwake, ili tumuonyeshe baadhi ya ishara zetu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.
Maana ya neno Israi katika lugha ya kiarabu ni kutembea usiku. Makusudio ya neno ‘mja wake’ hapa ni Muhammad (s.a.w.). Msikiti mtak- tifu ni ule ulioko Makka kwenye Al-ka’ba. Anasema mwenye Rawhul-lbayan na wengineo: “Riwaya iliyo sahihi zaidi ni kuwa safari ya Israi ilianzia kwenye nyumba ya Ummu Hani, dada yake Ali bin Abu Twalib.”
#SheikhOthmanMaalimKisachaIsrainaMiraji #KisachaIsrainaMiraji #mtumemuhammadisranamiraji
Msikiti wa mbali (Masjidul-Aqswa) ni hekalu la Nabii Suleiman. Umeitwa msikiti kwa sababu ni mahali pa kusujudu, kutokana na neno la Kiarabu masjid (msikiti) lenye maana ya mahali pa kusujudu. Na umeitwaMasjidul Aqswa (msikiti wa mbali), kwa sababu ya kuwa mbali na Makka. Msikiti huo umebarikiwa kandoni mwake kwa baraka za kidini, kwa vile ni nchi ya mitume na kwa baraka za kidunia kwa mito na miti. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.
Inawezekana ‘Yeye’ kuwa ni Mwenyezi Mungu kwa maana ya kuwa anamjua Mwenye kuamini na mwenye kukanusha tukio la Israi. Pia inawezekana kuwa ‘yeye’ hapa ni Muhammad (s.a.w.) kwa maana ya kuwa anajua ukuu na utukufu wa Mwenyezi Mungu.
Imesemekana kuwa Israi ilikuwa usiku wa kuamkia tarehe 27 Rajab (mfunguo kumi). Na pia imesemekana ilikuwa 17 Rabiul-awwal (mfunguo sita).
Sheikh Othman Maalim - Kisa cha Israi na Miraji
Теги
AlIhsaanFoundationKenyaRajaiAyoubRizwanulhaqQureshiIzudinAlwyAhmedMasjidIstiqaamahBujumburasharifyussufchannelDiamondPlatnumzWasafiMediaSimuliziNaSautiyofaveMiddlesimbaAlikibaOmmyDimpozRayvannyMbossoLavaLavaHarmonizeOtileBrownOfficialNyashinskiWillyPaulMsafiMillardAyoMuungwanaTvMCLDigitalMtanzaniaDigitalGlobalTVOnlineMwanaHALISITVNgasaTvUhondoTVAzamTVLilOmmyTVABCHABARIBekaFlavourEnockBellaRichMavokoWCBWASAFINavyKenzoMauaSamaDarassa