WACHIMBAJI wadogo wa madini hapa nchini, wamemwangukia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kuwaruhusu kuendelea na shughuli yao ya kusafirisha mchanga wenye madini ya Copper kwenda nje ya nchi na kuzuia mchanga wenye dhahabu kwa sababu haufanani.
Wakizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, wafanyabiashara hao wamesema kuwa wanamuomba rais awaangaalie kwa jicho la huruma kwani mchanga wenye madini ya dhahabu na wenye madini ya Copper na Nickel hutofautiana kwa hiyo kuzuia mchanga wote kumewasababishia usumbufu usiokuwa wa lazima.
Wakielezea malalamiko yao walisema kuwa baada ya tamko la rais kutolewa, hakuna shughuli yoyote inayofanyika katika migodi yao na hata bandarini pia kuna baadhi ya makontena yenye mchanga wa Nickel lakini nayo yamezuiwa na kusababisha waingie gharama kubwa ya kulipia gharama za makontena hayo kuhifadhiwa bandarini.
“Tunamwomba rais atuonee huruma kwani siku moja ikipita bila shughuli yoyote ya uchimbaji kufanyika huko mgodini gharama yake kwa siku ni takribani milioni nne kutokana na mikataba yetu tuliyoisaini juu ya shughuli nzima za uchimbaji,” alisema Thobias Rweyemamu.
Miongoni mwa wachimbaji na wasafirishaji wa mchanga huo waliojitokeza ni Salum Nassor (anayechimba madini ya Copper na Nickel Dodoma na Tunduma), King Suleiman (Mchimbaji wa madini na mnunuzi) na Thobias Rweyemamu (Mchimbaji wa madini ya Nickel katika mgodi wa Dodoma).
Ещё видео!