UONGOZI wa Simba umebainisha kwamba jitihada za kumbakisha nyota wao Clatous Chama ziligonga mwamba baada ya mchezaji huyo lkuomba kupata changamoto mpya.
Leo Agosti 16 baada ya tetesi kueleza kwamba Chama atakuwa ndani ya kikosi cha RS Berkane cha Morocco imetolewa taarifa rasmi kwamba Chama pamoja na mshikaji wake Luis Miqissone hawatakuwa sehemu ya kikosi hicho.
Crescentius Magori Mshauri wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurungezi ya Simba amesema kuwa hawakuwa na mpango wa kumuuza Chama ila yeye mwenyewe aliomba kuondoka na pesa ambayo wamewauza wachezaji hao ni ndefu mfano wake hakuna.
--
Dar24 ni chanzo namba moja cha habari kwa watanzania mahali popote walipo duniani. Kwa habari za uhakika kutoka nyanja mbali mbali tembelea www.dar24.com
#simbasc #clatouschama #usajili
Ещё видео!