Mgombea urais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi akitoa tathmini ya kampeni inayoendelea visiwani Pemba.
Dk Mwinyi alitoa tathmini hiyo mara baada ya kumaliza mazungumzo na mabalozi wa shina katika eneo la Micheweni, Kaskazini Pemba.
Mbali na tathmini hiyo pia alizungumzia namna zitakavyopatikana fedha za kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ambayo amekuwa akiwaahidi wananchi katika mikutano mbalimbali ya kampeni, iwapo wananchi watampa ridhaa ya kuongoza Serikali ya awamu ya nane.
Dk Mwinyi pia alizungumzia namna ya kutumia ardhi ndogo iliyopo visiwani kwa kilimo chenye tija.
Pia amezungumzia kuhusu mipango ya matumizi ya ardhi ya Bagamoyo ambayo Zanzibar ilipewa kwa ajili ya kufugia mifugo ambayo ingekuwa ikisafirishwa kuletwa Zanzibar.
Ещё видео!