GLOBAL HABARI: JPM, MSEKWA WAMLILIA KINGUNGE
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya Mwanasiasa mkongwe nchini Kingunge Ngombale-Mwiru aliyefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kushambuliwa na Mbwa wake.
Katika salamu hizo Rais Magufuli amemuelezea mzee Kingunge kama mtu aliyetoa mchango mkubwa kwa taifa katika maisha yake yote hapa duniani na kwamba aliipenda sana Tanzania.
Rais Magufuli amesema, amesikitishwa sana na kifo hicho na kwamba taifa limempoteza mmoja ya watu waliotoa mchango mkubwa katika maendeleo na ukuaji wa uchumi.
Taarifa kutoka kwa Mtoto Mkubwa wa Marehemu Kinje Ngombale Mwiru amethibitishaa kuwa Baba yake Mpendwa amefariki usiku wa kumakia leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.
Marehemu Kingunge Ngombale Mwiru amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95 na ameacha watoto kadhaa.
Subscribe muda huu www.youtube.com/user/uwazi1
Install #GlobalPublishersApp
Android: [ Ссылка ]
iOS: [ Ссылка ]
Subscribe [ Ссылка ]
FACEBOOK: [ Ссылка ]... TWITTER: [ Ссылка ] Visit [ Ссылка ], Subscribe [ Ссылка ] Kupata video nyingine za aina hii, subscribe kwenye chanell yetu kwa kubofya… [ Ссылка ] [ Ссылка ] [ Ссылка ] WEBSITE: [ Ссылка ] FACEBOOK: [ Ссылка ]... TWITTER: [ Ссылка ] INSTAGRAM: [ Ссылка ]..
Ещё видео!