Baada ya kikao cha kusikiliza kero za wafanyabiashara wa unga na mchele wilayani Kahama mkoani Shinyanga na mbunge wa jimbo la Kahama mjini Jumanne Kishimba kilichoketi jana Septemba 05, 2022 hatimae changamoto za wafanyabiashara hao zimepatiwa ufumbuzi.
Wakizungumza baadhi ya wafanyabiashara leo Septemba 06, 2022 kwenye kikao kilichowakutanisha wafanyabiashara, mbunge na halmashauri kwenye ukumbi wa halmashauri wafanyabiashara hao wamesema wamefurahishwa na muafaka walioufikia.
Wamesema changamoto ya tozo iliyokuwa inawakabili imetatuliwa hivyo watafanya kazi kwa kujiamini na kila mfanyabiashara atalipa ushuru bila shida na wamewashauri wafanyabiashara wenzao kuwa waaminifu.
Ещё видео!