Maamuzi yaliyotolewa na korti hivi majuzi kuwaruhusu wanandoa kutalikiana bila kuzingatia utaratibu wa kisheria yameonekana kuibua hisia tofauti miongoni mwa wakenya.
Kwa mujibu wa jaji Reuben Nyakundi wa mahakama ya Malindi, endapo mwanandoa ameashiria kutomtaka tena mwenzake na kujitoa kwenye ndoa hiyo kwa hiari na hata kuoa mpenzi mwingine, basi ndoa hiyo itatambuliwa kama iliyovunjika hata kama utaratibu ufaao wa kutalikiana haukuzingatiwa. Aidha wataalamu wa sheria wanasema ndoa iliyo na mizizi ya sheria haivunjwi pasi na utaratibu wa kisheria kufuatwa.
Ещё видео!