Mgombea ubunge jimbo la Moshi Mjini kwa tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema,Raymond Mboya amesema endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo hilo atahakikisha Hospitali ya kisasa ya Wilaya inajengwa katika jimbo hilo ili kuondoa adha ya huduma za afya ambazo wananchi wamekuwa wakikabiliana nazo.
Mboya ameyasema hayo leo Agosti 4,2020 wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ubunge wa jimbo hilo ambapo umefanyika katika eneo la manyema Manispaa ya Moshi.
Ameongeza kuwa, endapo atapewa ridhaa na wananchi wa mji huo kuwa mbunge wao ataenda kusimamia na kuhakikisha mji huo unatangazwa kuwa jiji kwani michakato yote imeshakamilika na kusema kuwa suala hilo kwake ni jepesi na ataenda kulipigania.
Ещё видео!