Mgombea ubunge jimbo la Moshi, kwa tiketi ya chadema Raymond Mboya, amesema,endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo atatumia kiasi cha fedha za mshahara wake kuboresha, makazi ya polisi, pamoja na vitendea kazi.
Mboya ameyasema leo septemba 7,2020,wakati akihutubia wananchi wa kata ya Mawenzi, viwanja vya stendi kuu ya mabasi Moshi mkoani kilimanjaro.
Amesema mbali na kuboresha makazi ya polisi pia kila mwezi atakuwa akitoa lita 150 za mafuta kwa ajili ya magari ya polisi.
Ещё видео!