UKIMWI ni ugonjwa sugu, unaotishia Maisha na husababishwa na Kirusi cha ukimwi (VVU)
Kirusi huyu huvamia kinga ya mwili na kuifanya iwe dhaifu kiasi cha kushindwa pambana na maradhi hivyo kufanya mtu augue magonjwa mbalimbali. Mwathirika anapopata magonjwa na dalili zake kutokana na kinga ya mwili kushindwa kufanya kazi kwa sababu ya VVU, hali hiyo hufahamika kama UKIMWI. Hivyo Tukisema UKIMWi tunamaanisha mwonekano wa dalili mbalimbali kwa mtu mwenye maambukizi ya VVU.
Matumizi ya dawa za VVU huweza kuzuia mwendelezo wa mgonjwa kupata dalili za UKIMWI
Dalili za awali
Dalili za awali za maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi ni pamoja na
Kupata dalili za mafua ndani ya wiki mbili toka umepata maambukizi inayoweza kudumu wiki kadhaa na kuondoka. Dalili zingine ni;
Homa
Maumivu ya kichwa
Maumivu ya misuli
Maumivu ya maungio ya mwili(jointi)
Harara
Koo kuwa kavu
Vidonda mdomoni vinavyouma
Kuvimba mitoki, haswa ya shingoni
Kuharisha
Kupoteza uzito(kupungua uzito)
Kikohozi(kukohoa)
Kutokwa jasho wakati wa usiku
Dalili hizi zinaweza kuwa za wastani na mtu anaweza asizishitukie.
Dalili za mwendelezo
Jinsi VVU vinavyozidi kuharibu mfumo wa kinga ya mwili, mwili utaanza kuonyesha dalili za UKIMWI zilizo sugu kama vile;
Homa
Mwili kuchoka
Kuvimba mitoki- kama dalili ya kwanza ya maambukizi
Kuharisha
Kupungua uzito
Maambukizi ya fangasi kooni
Mkanda wa jeshi
Nimonia (pneumonia)
Dalili za UKIMWI
Dalili za Mtu anayeelekea kupata UKIMWI au za mtu mwenye UKIMWI ni;
Dalili za UKIMWI mara nyingi huwa hazitokei kwa watu Wenye maambukizi ya VVU na tayari wamesha anza dawa mapema toka walipogundulika.
Endapo mtu hajapata dawa huchukua takribani wastani wa miaka 8 hadi 10 kupata dalili za UKIMWI
UKIMWI unapompata mtu Kinga za mwili huwa chini kiasi cha kutosha na hivyo mtu huweza kuambukizwa magonjwa mbalimbali na kuonyesha dalili za UKIMWI.
Dalili za UKIMWI ni pamoja na
Kutokwa jasho
Kutetemeka mwili(homa)
Homa za kujirudia
Tatizo sugu la kuharisha
Kuvimba mitoki na tezi
Tatizo sugu la Ulimi kuwa mweupe na fangasi wa kinywani
Kuchoka mwili kusikoelezeka na kusipokuwa na sababu ya msingi
Mwili kuwa dhaifu
Kupoteza uzito
Vipele na harara kwenye Ngozi
Kumbuka kuwasiliana na daktari wako kwa ushauri na tiba siku zote kabla ya kuchukua hatua yoyote baada ya kusoma makala hii.
Wasilina na daktari wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba zaidi kupitia kitufe cha mawasiliano yetu chini ya touti hii.
Video hii imejibu kuhusu
Zipi ni dalili za ukimwi?
Dalili za ukimwi huanza muda gani?
Dalili za ukimwi huchukua muda gani?
Dalili za gonjwa la UKIMWI?
Dalili za ukimwi?
Dalili za mepema za UKIMWI, dalili za HIV positive, dalili za HIV, Dalili za HIV/AIDS, dalili za haraka za UKIMWI
Ещё видео!