[ Ссылка ]
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi amesema asilimia kubwa ya watu wanatunza fedha ili ziwasaidie uzeeni na kusahau kutunza afya zao.
Janabi amesisitiza tofauti na kutunza afya hakuna kitu kitakachokuwa na manufaa uzeeni kama afya imetetereka ikiwamo fedha.
"Nafikiri ungetunza afya ikusaidie uzeeni kwa sababu fedha hizi zitakuja kukusaidia kulipia matibabu ya magonjwa hospitalini. Unafanya kazi miaka, unahangaika mjini miaka yote ili ukipata fedha uanze kuja kulipia betri za moyo nafikiri hiyo sio nzuri," amesema Profesa Janabi.
Janabi amesema hayo alipofanya mahojiano na vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam, huku akisema hajawahi kuwakataza watu wasile chakula, bali wasile ovyo na kula kwa wastani ili kuepuka magonjwa yasiyo ya lazima.
"Tunashauri kupunguza vyakula vya wanga na vyenye sukari.”
“Pia tunakataza ulaji wa vyakula vya kusindika, kwa sababu ili vikae muda mrefu kwenye shelfu lazima viwekwe kemikali, chumvi na sukari," amesema Profesa Janabi.
Ili kufahamu zaidi alichozungumza Profesa Janabi, usikose Jarida la Afya Februari 23, 2024 pia endelea kufuatilia gazeti la Mwananchi na mitandao yake ya kijamii.
Ещё видео!