Kamati kuu ya chama cha Mapinduzi CCM Taifa kimempitisha majina ya wagombea wawili katika jimbo la Konde visiwani Zanzibar na Ushetu wilaya ya Kahama ambapo Emmanuel Cherehani ameteuliwa kuwa mgombea ubunge jimbo Ushetu katika uchaguzi mdogo baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Elias Kwandikwa kufariki dunia na Mbarouk Habibu ameteuliwa kuwa mgombea jimbo la Konde
Ikumbukwe mwanzoni mwa mwezi agosti 2021 aliyekuwa mbunge wa jimbo la Ushetu wilaya ya Kahama na Waziri wa Ulinzi na jeshi la kujenga Taifa alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu mkoani Dar Es Salaam na badaye kuzikwa kwa heshima za kijeshi kijijini kwao Butibu Ushetu
Ещё видео!