Mkutano wa 12 wa bunge la 11 umehitimishwa juma hili jijini Dodoma ambapo zaidi ya maswali ya msingi 120 yaliulizwa.
Bunge hilo pia lilijadili miswada 5 na muswada kinara ulikuwa ni ule wa kujadili Dodoma kuwa Jiji. Sambamba na hilo wabunge pia walijadili mswada juu ya kuundwa kwa bodi ya kitaalam wa walimu ambao kwa sasa unasubiri sahihi ya Rais Magufuli ili kuwa sheria.
Kujadili hili, Mizani ya wiki imewamualika Katibu Mkuu CHAKAMWATA, Mwalimu Meshack Lupakisyo pamoja na Mwenyekiti Jukwaa la Waalimu Tanzania, Msafiri Mpendu.
Ещё видео!