Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Tanzania Bara Simba SC wamepoteza mchezo wa pili kwenye ligi hiyo msimu huu kwa kukubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Kagera Sugar.
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, Kagera ‘wamewapoteza’ Simba kipindi cha kwanza kwa kuonesha kandanda safi na kufanikiwa kupata mabao mawili yakifungwa na Kassim Khamis dakika ya 18 na Ramadhan Kapera dakika 41.
Simba walifanya mabadiliko kipindi cha pili kwa kuwatoa Haruna Niyonzima na James Kotei nafasi zao zikichukuliwa na John Bocco na Hassan Dilunga, mabadiliko ambayo yaliwasaidia kupata bao moja likifungwa na Emmanuel Okwi dakika ya 64.
Ushindi wa Kagera Sugar dhidi ya Simba SC leo umeibeba kutoka nafasi ya 17 hadi nafasi ya 13 baada ya kufikisha pointi 39 huku Simba ikiendelea kusalia kwenye nafasi ya tatu na pointi 60.
Ещё видео!