Mmiliki wa mgodi wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Mathias Lyatuu, amesema Mamlaka ya mapato nchini (TRA) inapaswa kufuata utaratibu unaotumiwa na wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini, wa kudai mapato pindi wachimbaji wanapopata madini.
Lyatuu ameyasema hayo kwenye kikao cha TRA na wamiliki wa migodi ya madini ya Tanzanite, kuhusiana na namna ya kulipa mapato kwa Serikali.
Ofisa huduma na elimu ya mlipa kodi wa TRA Mkoani Manyara, Joseph Massawe amesema wachimbaji wanapaswa kutunza kumbukumbu ya matumizi ya migodini ili kuweka mahesabu sawa pindi watakapozalisha madini.
Mmiliki mwingine wa mgodi Boniface Mgala amepongeza kutolewa kwa elimu hiyo kwa wamiliki wa migodi hiyo.
Ofisa wa huduma na elimu ya mlipa kodi wa TRA kanda ya kaskazini, Eugenia Mkumbo amewataka viongozi wa chama cha wachimbaji madini Mkoa wa Manyara (Marema) kuandika barua ya kuomba kuondolewa tozo za vibao vya majina ya umiliki wa migodi yao.
Ещё видео!