Watawa wametakiwa kumfuata Kristu kwa utulivu na ukamilifu ili kuishi vizuri katika kumfuata Kristu.
Hayo yamesemwa na Padre, Fredrick Lunyamaya, wa Shirika la Yesu na Uenezaji wa Injili na Paroko wa Parokia ya Nanjota Jimboni TUNDURU-Masasi kwenye Ibada ya
ya Adhimisho la Ibada ya Misa Takatifu iliyofanyika katika Kanisa la Masista wa Mungu Mwokozi la Mtakatifu Yakobo Mtume, Migongo Masasi.
Aidha, kwenye Ibada hiyo Masista sita (6) wameweka Nadhiri zao za Kwanza pamoja na Masista wapatao 17 ambao wamerudia Nadhiri zao Mbele ya Mama Mkubwa wa Shirika Regioni ya Tanzania, Mheshimiwa Sr. Yasintha G. Kalla, SDS
Ещё видео!