@partialyrics #tunategemeana
1 Kor 12:12
Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo.
1 Kor 12:20
Lakini sasa viungo ni vingi, ila mwili ni mmoja
GODFREY STEVEN ft IRENE UWOYA - TUNATEGEMEANA REMIX LYRICS
Wale wa ng'ambo wanauliza mmewezaje
Wale wa ng'ambo wanajibu mnashindwaje
Wale wa ng'ambo wanauliza mmevukaje
Na ng'ambo inajibu mnashindwaje
Mlichonacho hatuna
Tulicho nacho hamna
Basi tubadilishane
Tunufaike sote
Ulionalo gumu kwako
Kwa mwingine rahisi
Uonalo rahisi
Kwa mwingine ni gumu
Sababu kamwe mapito
Yanatofautiana
Tutiane moyo sote
Safari ni moja
Sababu ooh
Tegemeana
Tegemeana
Tunategemeana
Ili giza litoweke
Lahitaji mwanga ujue
Tena hakuna mrefu
Pasipo na mfupi
Ukiona daraja
Limejengeka ujue
Palionekana bonde
kabla ooh
Ulionalo gumu kwako
Kwa mwingine rahisi
Uonalo rahisi
Kwa mwingine ni gumu
Ещё видео!