Chama cha wataalamu wa afya nchini kinachojumuisha wahudumu wa afya kutoka nyanja mbalimbali za kimatibabu sasa kinashinikiza kwamba wahudumu elfu-10 zaidi wa afya waajiriwe ili kukomesha mzozo katika sekta ya afya. Kundi hilo linadai kwamba idadi ya wafanyikazi katika sekta hiyo inakumbwa na mzigo mkubwa na wakati umewadia kwa serikali kujaliza wahudumu walioko ili kusaidia kukabiliana na ongezeko la visa vya maambukizi ya virusi vya corona nchini. Chama hicho pia kinataka marupurupu kwa wale wanaokabiliana na ugonjwa wa COVID-19 yatolewe hadi mwezi Juni mwaka ujao wakidai kwamba athari za janga hilo zitahisiwa hadi baada ya mwaka huu.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: [ Ссылка ]
Follow us on Twitter: [ Ссылка ]
Find us on Facebook: [ Ссылка ]
Check our website: [ Ссылка ]
#KBCchannel1 #KBCNewsHour #KBClive
Ещё видео!