Leo July 9,2018 tunayo story kutoka kwa shirika la Dawasco ambalo limeamua kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji kwa ukamilifu.
Akizungumza na Ayo TV, Eng. Tyson Mkindi amesema Dawasco lina watu maalum wa kusimamia na kufatilia miundombinu yote pindi inapotokea hitilafu hata kama ni usiku.
"Ndio maana unaona tupo hapa maeneo ya Survey Dar es Salaam, muda huu wa saa 6 usiku tunarekebisha bomba kuu la maji linaloelekea Mjini Kati, maeneo ya Manzese, Magomeni, "amesema.
Eng. Tyson Mkindi amesema ukarabati wa bomba hilo unatokana na hitilafu iliyojitokeza katika maungio ya bomba na sehemu zinazoshikilia bomba hilo.
"Nawahakikishia hadi jioni maji yatarejea kama kawaida na niwatoe hofu tu kuwa hili sio tatizo la maji ila tunaziba bomba ambalo linavujisha maji kwa chini," amesema.
Ещё видео!