Rais William Ruto amepuuza semi za kinara wa Azimio Raila Odinga kuwa makamishna watatu wa IEBC wakiongozwa na mwenyekiti aliyeondoka Wafula Chebukati walimtembelea kwake kabla ya matangazo ya matokeo ya uchaguzi wa urais. Rais akisema ameshangaa ni kwanini ushahidi huu haukutolewa katika mahakama ya upeo wakati wa kuskizwa kwa kesi ya kupinga ushindi wake. Ruto akiendeleza shutma zake kwa viongozi wa Azimio kuhusu mikutano ya hadhara wanayoendesha akisema mfadhili wao alikuwa anataka kusambaratisha hatua yake ya kutaka kuhakikisha kila mkenya analipa ushuru.
Ещё видео!