Chuo cha ufundi Arusha kimetambua kituo cha kuzalisha umeme wa maji cha Kikuletwa kama eneo linalofaa kwa ajili ya uanzishwaji wa kituo cha mafunzo ya nishati ya umeme utokanayo na maji. ATC iliiomba serikali kumilikishwa kituo cha kuzalisha umeme cha Kikuletwa kutoka TANESCO (mmiliki wa wakati huo). Serikali liilikubali ombi la ATC kwa msajili wa Hazina kuidhinisha kuhamisha mali zote za kituo cha kuzalisha umeme cha Kikuletwa kwa chuo cha cha ufundi Arusha mnamo Julai 2012. Kwa upande mwingine, TANESCO ilikabidhi mali na haki zote za kituo cha umeme cha Kikuletwa kwa ATC mwezi Aprili mwaka 2013.
Kituo hiki cha Mafunzo kitatumika kama kitovu cha kuhudumia maendeleo ya sekta ya nishati ya umeme wa maji katika Tanzania. Katika uendelezaji wa kituo cha Kikuletwa shughuli zilizopangwa ni pamoja na: (i) Ukarabati na uendeshaji wa kituo cha kuzalisha umeme cha Kikuletwa, (ii) Kuanzishwa kwa kituo kitakachohusika na mafunzo na utengenezaji wa mitambo midogo midogo ya kuzalisha umeme (iii) Uongezaji wa uwezo wa kuzalisha umeme kwa kuendeleza maeneo mapya ktk mto Kikuletwa (cascading), (iv) Kuhifadhi mazingira yaliopo (v) Kujenga uwezo na kuendeleza wafanyakazi katika kila hatua ya mradi.
Ещё видео!