Watu kumi wanashikiliwa na jeshi la Polisi mkoa Arusha kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo wizi,uhamiaji haramu pamoja na madawa ya kulevya aina ya bangi.
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha ACP Salum Hamduni alisema kuwa mnamo tarehe Desemba 30,2020 saa nne asubuhi katika eneo la Olnjavitian kata ya Sombetini Halmashauri ya jiji la Arusha jeshi hilo lilifanikiwa kumkamata Ibrahim Ezekiel mkazi wa Mianzini akiwa na vitu mbalimbali vya wizi pamoja na vifaa vya uvunjaji.
Kamanda Hamduni alieleza kuwa mtuhumiwa mwingine wa wizi akikamatwa Desemba 29,2020 saa mbili usiku maeneo ya Uswahilini katika Kata hiyo ni Zuberi Juma ambapo badhi ya vifaa hivyo ni pamoja na TV,Laptop, Tablet ,Compressor, pasi, dryer, radio, spika, ving'amuzi,Subwoofer pamoja na vitu vingine vingi.
Ещё видео!