GLOBAL HABARI JAN 16: WAZIRI AKERWA NA UJENZI WA KIWANDA, ATOA MAAGIZO MAZITO..
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu) Jenista Mhagama amesema Serikali haijaridhika na kasi ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Karanga katika Gereza la Karanga Mkoani Kilimananjaro na kumtaka mkandarasi kuikamlisha kazi hiyo kabla ya tarehe 2 Februari mwaka huu.
Akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo Waziri Mhagama amesema hakuna sababu kwa mradi huo kutokamilika kwa wakati kwani fedha zote zilizohitajika katika hatua muhimu za mradi huo zimekwishatolewa.
Waziri Mhagama amesema kiwanda hicho ni miongoni mwa miradi muhimu ya kimkakati iliyopangwa kutekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano, hivyo mkandarasi hana budi kuzingatia masharti ya mkataba uliowekwa ili kuhakikisha kuwa kiwanda hicho kinakamilika kwa wakati na kuweza kuleta tija iliyokusudiwa.
Kwa upande Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Magereza Nchini, Hamis Nkubasi amesema Jeshi hilo limepokea maelekezo yote ya Serikali na imejipanga kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika kwa wakati ili kuweza kufikia malengo yaliyowekwa.
#GLOBALHABARI
GLOBAL TV ONLINE ( +255 784 888982)
HABARI MPYA DAILY:
[ Ссылка ]...
HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA:
[ Ссылка ]...
GLOBAL RADIO TV:
[ Ссылка ]...
EXCLUSIVE INTERVIEW:
[ Ссылка ]
Ещё видео!