Zaidi ya wanafunzi milioni 3.5 humu nchini watakosa kurejelea masomo shule zitakapofunguliwa mwezi januari kutokana na makali ya njaa. Ripoti ya shirika la Save the Children inasema kuwa zaidi ya watoto milioni mbili walio na umri wa kati ya miaka minne hadi kumi na saba hawakuhudhuria masomo muhula wa tatu kwa sababu ya ukame. Wengine milioni 1.6 wako katika hatari ya kuacha shule muhula ujao huku ukame ukizidi kuathiri kaunti 31. Kaunti za Mandera, Garissa, Wajir, Turkana, Marsabit, Narok, Pokot Magharibi na Samburu ni miongoni mwa kaunti zilizoathirika zaidi huku Mandera ikiongoza kwa idadi ya watoto walio na umri wa miaka minne hadi kumi na saba ambao hawajahudhuria masomo muhula wa tatu.
Ещё видео!