RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amewahakikishia wananchi kuwa Serikali ina mipango thabiti, Madhubuti na mizuri ya kupata fedha kwaajili ya maendeleo zaidi.
Ameyasema hayo alipoweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara za juu (Flyover) ya kwanza Zanzibar kwa awamu ya mwanzo, Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi ikiwa ni ufunguzi wa shamrashamra za miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema, uzinduzi wa ujenzi wa (Flyover) hiyo ni mwendelezo wa kukamilisha ahadi na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ambayo imevuka malengo kwa mafaniko makubwa ya ujenzi wa miradi ya maendeleo.
Rais Dk. Mwinyi amefahamisha kuwa ujenzi huo wa Flyover ni mwanzo wa mambo makubwa zaidi yanayokuja na kueleza Serikali inampango wa kujenga mradi mkubwa wenye makutano ya barabara nne za juu (Interchange Road) na kuwasisitiza wananchi kuendelea kuiunga mkono Serikali yao.
Aidha, Dk. Mwinyi ametoa indhari kwa wananchi kuwa na nidhamu ya matumizi ya hifadhi ya barabara kwa kuanchana na ujenzi wa kiholela wa makaazi na shughuli nyengine za jamii pembezoni mwa barabara.
Ameeleza hifadhi za barabara zimewekwa kwaajili ya kupitisha miundombinu mengine ikiwemo njia za maji, umeme, mawasiliano na mitaro ya maji machafu.
Rais Dk. Mwinyi pia amewasihi wanasiasa, viongozi wa umma na binafsi kuwa na uongozi wenye kuacha alama kwa kuweka maendeleo yenye kuacha historia kwa vizazi vya baadae.
Akizungumzia kaulimbiu ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar isemayo “Amani, Umoja na Mshikamano kwa Maendeleo yetu”, Rais Dk. Mwinyi amewasihi wananchi kuendeleza amani na mshikamano uliopo kwa lengo la kuiendeleza nchi kwa maendeleo.
Aidha, ameipongeza Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kwa kazi nzuri wanayofanya ya ujenzi wa miundombinu ya barabara, madaraja na mawasiliano.
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Dk. Khalid Salum Mohamed, amewasilisha shukurani za wananchi wa Zanzibar kwa Rais Dk. Mwinyi wanaompongeza kwa shughuli kubwa za maendeleo anazozifanya. Pia Dk. Khalid amezipongeza juhudi za Dk. Mwinyi za kuendelea kuiletea nchi Maendeleo.
Naye, Naibu Katibu mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasilianio na Uchukuzi, Makame Machano Haji, amesema ujenzi wa mradi huo hadi kukamilika kwake, utagharimu dola za kimarekani milioni 19 na takribani shilingi bilioni mbili zimetumika kwaajili ya kuwalipa fidia wananchi waliopisha mradi huo. Aliouelezea kuwa utapunguza msongamano wa vyombo vya usafiri katika makutano ya barabara za Mwanakwerekwe.
Akitoa salamu za Mkoa mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Idriss Kitwana amemshukuru Rais Dk. Mwinyi kwa kuupa hadhi na heshima kwa miradi mikubwa ya maendeo viwanja vya ndege vya kimaifa, masoko ya kisasa, Fyiover ya Mwanza baada ya miaka 61.
Amewasisitiza wananchi kuendelea kumuunga Mkono Rais Dk. Mwinyi ili awaletea maendeleo zaidi.
Ещё видео!