Picha ni abiria wakishuka kutoka katika kivuko MV. KOME II kinachotoa huduma kati ya Nyakaliro na Kome Halmashauri ya Mji Buchosa Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza. Kivuko hicho cha Tani 40, kina uwezo wa kubeba abiria 120 pekee.
Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) inajenga kivuko kipya ambacho ukubwa wake utakuwa mara nne
zaidi ya ukubwa wa kivuko kilichopo hivi sasa, kivuko hicho kipya kitakuwa na Tani 170, uwezo wa kubeba abiria 800 na magari madogo 22, kinakwenda kuondoa adha wanayokumbana nayo wakazi wa maeneo hayo baada ya kivuko MV.KOME II kuonekana kuzidiwa na uwingi wa abiria.
Ещё видео!