UFAFANUZI WA UHAKIKA WA TANZANIA KUTWAA MEDALI KATIKA NDONDI
Bondia Yusuf Changalawe afafanua kuhusu uhakika wa yeye kupata medali hata kama atashindwa kwenye mchezo wake wa nusu fainali Jumamosi na bondia wa Scotland.
Jana jioni Changalawe amefanikiwa kuigia hatua ya Nusu Fainali baada ya kumshinda kwa RSC (Referee stops the contest) katika round ya 1, Dakika ya 2:18* dhidi ya mpinzani wake Arthur Langelier kutoka nchi ya St. Lucia katika bout no. 119 ya uzani wa Light heavyweight 75kg - 80kg* .
Changalawe ameandika historia mpya ya medali katika ngumi baada ya miaka 24 ambapo Tanzania ilipata medali ya dhahabu kupitia Bondia Marehemu Michael Yombayomba mwaka 1998 katika Michezo ya Jumuiya ya Madola iliyofanyika Kuala lumpar, Malaysia.
Changalawe atapigana hatua ya Nusu fainali siku ya Jumamosi tarehe 6-08-2022 dhidi ya S. Lazzerini kutoka Scotland.
Katika Ngumi mshindi wa kwanza anapata medali ya Dhahabu, wa pili medali ya Fedha na watakaopoteza katika hatua ya nusu fainali watapata medali za Shaba katika kila uzani.
Ещё видео!