Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Dar es Salaam imempa tuzo Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuidhinisha maboresho ya mitaala ya elimu nchini ili kuendana na mahitaji ya wakati huu kwa lengo la kuharakisha maendeleo ya nchi na wananchi kwa ujumla.
Akikabidhi tuzo hiyo kwa waziri wa elimu Profesa Adolf Mkenda aliyepokea kwa niaba ya Rais, mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Khadija Ally Said amesema maboresho makubwa ya mitaala ya elimu kwa ngazi zote za elimu na taaluma zitaijenga Tanzania bora yenye wasomi wenye tija na ushindani kwenye soko la ajira na uzalishaji mali wa kujitegemea ikiwemo ujasiriamali.
Imeandaliwa na Ahimidiwe Olotu.
Ещё видео!