Uongozi wa Shule ya Sekondari Ivumwe, inayomilikiwa na Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), umemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kusaidia Sh milioni 40 kukamilisha ujenzi wa maabara tatu mpya na za kisasa.
Akizungumza leo Januari 1, 2025, Mkuu wa Shule hiyo, Oscar Mwaihabi, amesema shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma lakini inakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa miundombinu, hususan maabara.
Mwalimu wa masomo ya sayansi, Mrisho Mbombwe, amesema kukosekana kwa maabara kunarudisha nyuma maendeleo ya wanafunzi kwa kuwaelimisha kwa nadharia pekee badala ya vitendo.
Upande wake, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Wilaya ya Mbeya, Abdul Komba, ameahidi kulifikisha ombi hilo kwenye kamati ya siasa ya chama ili kuhakikisha mwaka 2025 unakuwa wa mafanikio.
Shule ya Sekondari Ivumwe, inayotoa elimu kwa kidato cha kwanza hadi cha sita, inamilikiwa na Jumuiya ya Wazazi wa CCM, ambayo Mwenyekiti wake ni Rais Samia Suluhu Hassan.
Ещё видео!