🔴#LIVE: GLOBAL HABARI DES. 03 - BILIONI 4 ZATENGWA KUIMARISHA MIUNDOMBINU JANGWANI DAR ES SALAAM
Serikali kupitia Mfuko wa Barabara (Road fund) imesema kuwa ipo tayari kupitisha kiasi cha shilingi bilioni nne kwa ajili ya kumlipa mkandarasi atakaepatikana ili kuboresha miundombinu ya jangwani mara baada ya uhakiki wa makisio hayo kukamilika na kujiridhisha.
Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa Bodi ya mfuko huo, Mwenyekiti wa Bodi Joseph Haule, amesema kuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha inatatua changamoto hiyo haraka kabla ya mvua za masika kuanza.
Aidha Haule ameongeza kuwa nia ya Bodi ni kuona wananchi na wasafirishaji wanatumia muindombinu hiyo wakati wote wa mvua na kiangazi katika majukumu yao ya kila siku
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Elius Mwakalinga, amesema kuwa Serikali kupitia Wizara yake imeandaa mkakati wa muda mrefu kuhusu miundombinu hiyo ambapo amesema kuwa kwa sasa wataalamu wanafanya usanifu wa kina kwa ajili ya kuja na suluhisho la kudumu ikiwemo ujenzi wa daraja lenye urefu wa mita 300.
Naye, Meneja wa TANROADS mkoa wa Dar es salaam, Mhandisi Julius Ngusa, amethibitisha kuwa ofisi yake inaendelea kuhakikisha kuwa michanga inayotuama katika eneo hilo inatolewa kwa wakati ili kuruhusu magari kuweza kupita mara baada ya mvua kunyesha.
⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:
⚫️ ANDROID:[ Ссылка ]
⚫️ iOS:[ Ссылка ]
⚫️ VISIT AMAZON: [ Ссылка ]
⚫️ JE, NA WEWE UNA HABARI?
⚫️ WASILIANA NA GLOBAL TV ONLINE ( +255 784 888982), ( +255 713 837506)
⚫️ Email: globaltvbest@gmail.com OR abbymrisho@gmail.com
⚫️ OUR PLAYLISTS:
⚫️ HABARI MPYA DAILY:shorturl.at/mnux2
⚫️ HISTORIA ZA VIONGOZI ZA KUSISIMUA: [ Ссылка ]
⚫️ GLOBAL RADIO TV: [ Ссылка ]
⚫️ EXCLUSIVE INTERVIEW: [ Ссылка ]
⚫️ Subscribe Global TV [ Ссылка ]
Ещё видео!