Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki Kuu la MBEYA Mhashamu GERVAS NYAISONGA amewataka waamini kutambua kuwa Ekaristi Takatifu (yaani mwili na damu ya Bwana wetu YESU KRISTO) ni ishara ya umoja kati yao na KRISTO, napia ni ishara ya umoja ya kati yao wao kwa wao kwa kuwa wanachota chemchemch kutoka kwake KRISTO YESU.
Askofu Mkuu NYAISONGA ambaye pia ni Rais wa Baraza la maaskofu katoliki TANZANIA ameeleza hayo kupitia homilia yake kwa Waamini walioshiriki Adhimisho la Misa Takatifu ya sherehe ya Mwili na Damu ya YESU iliyoadhimishwa Juni 14 katika Kanisa Kuu la Mt ANTONY wa PADUA jimboni MBEYA.
Amesema kuwa Ekaristi pia nikifungo cha mapendo, lakini inapungua utukufu wake kama wanaoshiriki wametindikiwa mapendo, kwa kuwa Ekaristi na mapendo daima vinakwenda pamoja na ndio maana Mtume PAULO alikuwa mkali sana kwa Wakorinto pamoja na wale aliowahubiria baada ya kuona wanatumia vibaya fursa ya Adhimisho la Ekaristi kutangaza utajiri wao na kuonyesha uwezo wa kifamilia.
Aidha Askofu Mkuu NYAISONGA ameongeza kuwa Waamini waendelee kuithamini, kuipokea na kuheshimu Ekaristi Takatifu pamoja na kwamba inaonekani katika umbo dogo la mkate na Divai, kwa kuwa humo yumo YESU mwenyewe na aliamua kubali kwa waamini kwa njia hiyo na alifanya hayo yote kwa mapenzi yake kwao.
Hata hivyo amewataka waamini kuacha kuichezea Ekaristi Takatifu, ikiwemo kuipokea bila ya kufanya maandalizi ya kiroho pamoja na malipizi, ambapo wengine wanaipokea huku mioyo yao ikiwa michafu, mikono yao ikiwa michafu na hata wengine wanadiriki kuiachanganya na mambo ya kishirikina.
Ещё видео!