Wengi hawaamini kama tatizo la gesi linatibika, wamekuwa wakilalamika kuhusu tatizo la gesi tumboni na limekuwa likisumbua sana, wengine mpaka matumbo yamevimba/yamejaa kama vitambi kwasababu ya tatizo hili hili, na wengine hawali vyakula vingi kwasababu wanaogopa gesi,
Tiba ipo 👉[ Ссылка ]
Hizi ni miongoni mwa sababu zinazo pelekea mtu kupata tatizo la gesi tumboni.
Matatizo kwenye Mmeng’enyo wa Chakula
Magojwa kama Ulcerative colitis, celiac disease na IBS-inflammatory bowel syndrome husababisha kujaa gesi kwa tumboni
Maji kubakizwa mwilini (fluid retention)
Wakati fulani maji yanaweza kubabakizwa kwenye sehemu fulani za mwili kama kweye magoti, tumboni na kwenye nyonga. Maji haya husababisha maumivu makali kwenye joints na tumboni. Uwepo wa maji tumboni hujulikana kama ascites na inaweza kuashiria kwamba una tatizo kwenye ini au maambukizi ya bacteria.
Ndio maana kuna umuhimu wa kufanya vipimo kama una homa ya ini (hepatitis B). kama kuna shida ya ini basi utapata dalili zingine kama kichefuchefu, macho na ngozi kuwa njano, kupungua uzito, kutapika damu na chakula kutosagwa tumboni.
Mwili kukosa maji (Dehydration)
Mwili unapokosa maji hufanya uchakataji na usagaji wa chakula kuwa mgumu. Mwili unapokosa maji ya kutosha hufanya kazi ya kuvuta na kuhifadhi maji mengi zaidi pale utakapokunywa maji ili kuepuka kutokea kwa upungufu huu. Maji yanapokuwa machache ndipo sasa unaweza kupata choo kigumu ama kukosa choo. Hakikisha unakunywa maji mara nyingi zaidi kila siku ili kuepuka tumbo kujaa gesi.
Kukosa choo ama kupata choo kigumu/Constipaton (kiungulia)
Constipation inaweza kuwa sababu kubwa ya kwanini tumbo lijae gesi. Constipation inaweza kusababisha choo kigumu, maumivu tumboni na kukosa choo kwa muda mrefu. Kukosa choo na choo kigumu husabishwa na ulaji wa vyakula vilivyokobolewa sana visivyo na fibre au kambakamba, matumizi kidogo ya maji, msongo wa mawazo na kuishi bila kufanya mazoezi.
Mzio wa chakula/vyakula
Mzio wa vyakula mbalimbali kama maziwa, mayai na ngano vinaweza kuwa ni sababu ya kujaa gesi kwa tumbo lako. Kuna aina nyingi ya vyakula inaweza kusababisha upate mzio. Cha kufanya sikiliza mwili wako unasemaje pale unapokula chakula. Kama mwili unakataa aina fulani ya vyakula na unapata mcharuko kama kuvimba, kuharisha, ama kutapika basi usitumie chakula hicho.
Maambukizi
Kama mwili unapambana na maambukizi aidha ya bacteria, virusi, fangasi au vimelea wengine basi unaweza pata tatizo la kujaa gesi tumboni.
Majeraha Kwenye Mfumo wa Chakula
Wakati mwingine unaweza kupata gesi tumboni kutokana na vidonda ama uvimbe kwenye baadhi ya sehemu za mfumo wa chakula kama utumbo mdogo na utumbo mpana. Uvimbe unaweza kuzuia utolewaji wa uchafu na kufanya gesi na maji kukwama.
Mabadiliko ya Homoni (wanawake)
PMS (pre menstrual syndrome) ikimaanisha mkusanyiko wa dalili zisizo za kawaida za kipindi cha hedhi ni chanzo cha tumbo kujaa gesi. Tatizo linaweza kuwa kubwa kama una uvimbe kwenye kizazi na hedhi yako inavurugika. Kwanini wanawake hupata gesi tumbo wakati au karibia na kipindi cha hedhi? Mwanamke anapokaribia hedhi kiwango cha homoni ya estrogen huongezeka na ukuta wa mfuko wa mimba kuongezeka. Pale anapopata siku zake basi damu na maji mengi hutolewa nje na hivo tumbo kurudi katika hali ya kawaida.
Saratani
Moja ya dalili za saratani ya utumbo mpana na saratani ya mfuko wa mimba ni tumbo kujaa gesi. Ndio maana ni muhimu kuongea na daktari wako pale ambapo umejaribu kila njia ya kundoa tatizo lako lakini bado halijaisha.
Vyakula vya Kuepuka pale Unapotaka Kutibu Tatizo la Tumbo Kujaa Gesi
Vyakula vya sukari na snacks zilizooongezewa utamu,
Nafaka na vyakula vya nafaka hasa ngano, mbaazi na Maharage huongeza uzalishaji wa gesi tumboni
Vinywaji vilivosindikwa kama soda (Carbonated drinks), hivi ni vya kuepuka.
Pendelea kunywa chai yenye tangawizi yenye sukari kidogo au isiyo na sukari kabisa, ukipata asali ni bora zaidi uweke katika chai hiyo, na jitahidi kila siku ule punje tatu za vitunguu saumu,
Usisahau kunywa maji mengi kadri utakavyo jaaliwa na kufanya mazoezi japo ya yoga ni muhimu sana.
Katika kutibu tatizo la gesi tumboni zipo njia nyingi, mimi nimeeleza zile za asili ambazo ndizo ninaziamini na ni rahisi maana kila mmoja anaweza kuzifanya akiwa nyumbani kwake,
Dawa hizo zinapatikana katika maeneo yetu, fuatilia kwa umakini maelezo katika video hii na uchague dawa unayoona ni rahisi kwako kuifanya, na pia zinazidiana nguvu kulingana na mwili wa mtu hivyo nakushauri dawa moja uliyochavua ikishindwa jaribu nyingine.
Bonyeza hapa 👉[ Ссылка ]
#gas #gesitumboni #ulcer #vidondavyatumbo
Ещё видео!