[ Ссылка ]
Watu watatu wamefariki baada ya kunywa pombe haramu eneo la Kibera, waliouziwa na mtu mmoja anayefanya kazi katika afisi ya chifu. Swali ibuka hapa ni je maafisa wa serikali eneo la kibera wamebuni makundi ya kuuza pombe haramu? Inadaiwa jamaa huyo kwa jina wilson mutua huandamana na maafisa wa polisi katika misako ya kunasa pombe haramu, lakini badala ya kuimwaga, mshukiwa huichukua pombe mikononi mwa polisi na kuwauzia tena wenyeji wa kibera.juhudi zetu za kubaini iwapo kuna uhusiano kati ya mshukiwa huyo na maafisa wa usalama, katika biashara hii, ziliambulia patupu baada ya mutua kutiwa nguvuni dakika chache baada ya watu hao kufariki
Ещё видео!