Baadhi ya wabunge wa Wiper sasa wanamuonya kinara wao Kalonzo Musyoka, kwa kile wanasema ni juhudi zozote za kukubali ushawishi na kuondoka muungano wa OKA na kumuunga mkono kinara wa ODM Raila Odinga kwenye uchaguzi ujao. Viongozi hao wakiongozwa na Seneta Enock Wambua wanasema kuwa ni ujumbe wa watu wa Ukambani kwa Kalonzo kusimama imara na kupeperusha bendera ya urais kuingia Ikulu. Sasa wakimtaka Kalonzo kusalia kwenye muungano wa One Kenya Aliance pamoja na wenzake ili kuzuia mtafaruku wowote
Ещё видео!