Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango amewataka Wizara ya madini nchini na Tume ya Madini nchini kusimamia Wachimbaji wadogo waliyopata leseni wakawekeza mitaji Yao wasinyanganywe maeneo kwa kisingizio walipewa kwenye maeneo ya Wachimbaji wakubwa..
Amesema hayo jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya Wiki ya Madini Mwaka 2024 yaliyoandaliwa na Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania FEMATA.
Amesema amepokea malalamiko kadhaa kuhusu hilo la kuutoondolewa mchimbaji mdogo katika eneo la uchimbaji kwaajili ya kumpisha Wekezaji mchimbaji wa madini wakubwa.
Alisema hilo ni jambo lisiloeleweka la kumpatia leseni na baada ya kuwekeza ananyang'anywa leseni na anayemnyang'anya ni mamlaka Ile Ile iliyompa leseni
"Sasa hii linaleta hisia na uwezekano wa uwepo wa rushwa kwahiyo Waziri ulisimamie"
Dkt. Mpango amesema Serikali imeendelea kutenga maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo na kurasimisha maeneo yenye milipuko wa madini (rush). Nimeambiwa kuwa, katika kipindi cha Julai 2023 hadi Machi 2024, Tume ya Madini ilitoa Leseni za Uchimbaji Mdogo (PMLs) 6,934; Biashara (BLs)1,616;
"Leseni za Uchenjuaji wa Madini (PCLs) 35. Ongezeko hilo la utoaji wa leseni ni matokeo ya uhamasishaji wa uwekezaji uliofanywa katika Sekta ya Madini". Alisema Dkt Mpango.
"Hii inaonesha juhudi kubwa za Serikali katika kuwajali wachimbaji wadogo wa madini. Hata hivyo, nimeelezwa kuwa Wizara imefuta leseni 2648 zilizokutwa na makosa mbalimbali na maeneo kuwa wazi kwa waombaji wengine" alisema.
"Natumia fursa hii kuwasihi wachimbaji wote, waongezaji thamani na wafanya biashara wa madini, waendelee kufuata sheria ili kuepuka usumbufu mbalimbali ikiemo kufutiwa leseni za Madini. Nimeelezwa pia kuwa, wachimbaji wadogo wanamalalamika kuhusu tozo mbalimbali zinazotozwa na halmashauri mbalimbali.
Nawaomba halmashauri zote za wilaya na miji, ziandae sheria ndogondogo (by-laws) ambazo hazikinzani na Sheria ya Madini ili kuona namna bora ya kuweka tozo hizo.
Aidha, nitoe rai kwa Halmashauri zote zenye migodi kuitumia fursa za uwepo wa migodi katika maeneo yao kwa kuyatumia mapato yanayopatikana kama chachu ya kuleta maendeleo yenye tija kwa kizazi cha sasa na cha baadae.
Nashauri Halmashauri kuendelea kuwa wabunifu katika kubuni miradi hasa inayowawezesha wananchi katika kujipatia kipato ili kuongeza mzunguko wa fedha na kuleta maendeleo endelevu kwa kuwa rasilimali madini kuna siku zitakwisha.
Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya biashara ya Madini kwa kuanzisha Masoko 42 na vituo vidogo 100 vya uuzaji madini katika maeneo yenye madini nchini ambapo Soko la kwanza lilifunguliwa mkoani Geita.
Aidha, Serikali imeendelea kuhamasisha shughuli za uongezaji thamani madini ambapo hadi sasa jumla ya viwanda vitatu vya kusafisha dhahabu (Gold Refineries) vyote kwa pamoja vinauwezo wa kusafisha dhahabu kilogramu 515 kwa siku.
Viwanda hivyo vipo katika Mikoa ya Geita, Mwanza na Dodoma na vinafanya kazi.
Akiwa katika Banda la Maonyesho la bank ya NMB Mkuu wa idara ya Biashara wa bank ya NMB Alex Mgeni amesema Bank hiyo imekweisha toa mikopo ya zaidi ya shilingi bilioni 43 kwa wachimbaji wadogo kwa kushirikiana na FEMATA huku bank hiyo ikiendelea kuboresha huduma zake hasa kwa sababu changamoto iliyopo kwa wachimbaji wadogo ni elimu ilikujua umuhimu wa utunzaji wa fedha na kuwapa elimu ya utunzaji wa mazingira.
Awali Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania FEMATA John Bina alipongeza na kushukuru kwa ushirikiano mkubwa wachimbaji wadogo wanaopata serikalini tofauti na ilivyo katika mataifa mengine jinsi wachimbaji wadogo wanavyopewa ushirikiano na serikali zao.
Alisema taifa hili uongozi wa juu wa serikali kuu kukaa na kujadiliana hata kufanya maamuzi ya manufaa ya wachimbaji wadogo ili wapate tija katika uchimbaji wao nchini.
+++++++
Ещё видео!