#Dr_Mniko
Kama kitu kitaingia na kung’ang’ania ndani ya sikio lako kinaweza kusababisha usumbufu na kusababisha ushindwe kusikia kwa kitambo kama kitaziba njia nya sikio. Kama ni kitu chenye ncha kali kinaweza kutoboa ngoma yako ya sikio. Watoto wadogo wakati fulani wanaweza kuweka vitu masikioni, vitu kama mbegu, vidude vya kuchezea au vipande vya karatasi. Kama haujawaona wanaweka hivi vitu masikioni inaweza kuwa ngumu kujua kuwa wameviweka mpaka utakapoona wanalalamika kuwa wana maumivu masikioni, kuna uchafu unatoka masikioni au kama wanashindwa kusikia vizuri. Watu wazima pia huwa wanabakiza vipande vya pamba kwenye masikio wakiwa wanasafisha masikio yao (utaratibu huu wa kusafidha masikio kwa kutumia vijiti vyenye pamba haushauriwi na madaktari, ni utaratibu mbovu na wenye madhara). Kwa mara chache wadudu wanaweza kuingia na kukwama ndani ya masikio, hii inaweza kushtua, hasa kwa mtoto.
_____________________________________________________________________
TEMBELEA TOVUTI YETU KUJIFUNZA ZAIDI
*Website:[ Ссылка ]
TUFUATILIE KWENYE MITANDAO YA KIJAMII
*Facebook:[ Ссылка ]
*Instagram:[ Ссылка ]
*Twittwer:[ Ссылка ]
MUSIC CREDIT
* [ Ссылка ]
Ещё видео!