Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ameitaka Mamlaka ya Bandari nchini (TPA) kuhakikisha miradi yote ya maboresho ya bandari ya Tanga inakamilika ifikapo mwezi Aprili 2023 ili bandari hiyo ianze kufanya kazi kwa ufanisi na kuruhusu meli kubwa zaidi kuanza kutumia bandari hiyo.
Makamu wa Rais amesema hayo alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Gati mbili pamoja na uongezaji kina kutoka mita 3 hadi 13
unaondelea katika Bandari ya Tanga.
Amesisitiza ni lazima bandari hiyo iweze kufanya kazi kwa viwango na kuvutia zaidi watumiaji wa bandari katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Pia amemuagiza Meneja wa Bandari ya Tanga kushughulikia haraka
malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara kuhusu utendaji wa bandari hiyo
ikiwemo kuchukua muda mrefu utokaji wa mizigo inayopita katika bandari
hiyo ikilinganishwa na bandari nyingine za jirani.
Amesema mapungufu hayo katika bandari ya Tanga yamepelekea wafanyabishara kutumia bandari za nchi Jirani na hivyo kulikosesha taifa mapato ambayo yangetumika kuwahudumia wananchi.
Follow us on:
FACEBOOK;
SpotiLeo: [ Ссылка ]...
HabariLeo: [ Ссылка ]
DailyNews: [ Ссылка ]
INSTAGRAM;
HabariLeo: [ Ссылка ]...
SpotiLeo: [ Ссылка ]...
TWITTER;
Twitter HabariLeo: [ Ссылка ]
Ещё видео!