Aliyekuwa Mjumbe wa kamati kuu na Mwenyekiti wa masuala ya Kimataifa ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Lazaro Nyalandu amewataka wafuasi wa Chadema kumpigia kura mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Frolence Samizi.
Nyalandu ametoa kauli hiyo leo Mei 14, 2021 katika kilele cha kampeni za ubunge wa jimbo la Muhambwe zilizofanyika katika uwanja wa Taifa uliopo wilayani Kibondo mkoani Kigoma ambapo amesema wafuasi wa vyama vyote wanatakiwa kumchagua mgombea wa CCM.
Akinukuu maneno kutoka kwenye kitabu kitakatifu cha Biblia, Nyalandu amesema alipokuwa Chadema nyimbo zilikuwa haziimbiki, akimaanisha mambo yalikuwa hayaendi kama Kmaati ya Chama hicho ilivyokuwa ikiyapanga.
Ещё видео!