Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa Jean Pierre Lacroix leo ameanza ziara ya siku tatu nchini Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo DRC, kumuwakilisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. Ziara hiyo imeanzia Bunia Mashariki mwa DRC ambako amezuru kambi ya wakimbizi wa ndani Roe, kuzungumza nao na kushuhudia hali halisi lakini pia kuzungumza na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa. Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ni miongoni mwa walioambatana na Lacroix ametuandalia taarifa hii.
#HabarizaUN #UmojawaMataifa #Kiswahili #UNNewsKiswahili
Ещё видео!