siku moja tu baada ya watu kumi na saba kufariki huko nyahururu baada ya kunywa pombe aina ya yokozuna, watu wengine saba wamefariki katika eneo la ruiru gatabaya baada ya kunywa pombe hiyo haramu. Vifo hivi vya kutatanisha vinaashiria kwamba kuna haja ya wadau kushughulikia swala la unywaji wa pombe haramu ili kusitisha maafa zaidi. Wakati huo huo mwanaharakati mmoja anayeshughulikia maswala ya matumizi ya pombe na mihadarati alisema kuwa kuna haja ya kudhibiti sheria za mututho na kuzipa uwezo kamilifu wa kukabiliana na unywaji wa pombe haramu kiholela
Ещё видео!