Mbunge wa jimbo la Makete mkoani Njombe, Festo Sanga ni miongoni mwa Wabunge waliochangia hoja ya dharura iliyowasilishwa bungeni jijini Dodoma na Mbunge wa jimbo la Kilindi mkoani Tanga, Omari Kigua kuhusu suala la kupanda kwa bei ya mafuta.
Katika mchango wake pamoja na mambo mengine Festo ametaka kupunguzwa kwa tozo kwa udharura uliopo ili kunusuru msalaba wa ugumu wa maisha ya Watanzania hivi sasa na ametaka Serikali itafute fedha mahali pengine kwa ajili ya kuweka ruzuku kwenye mafuta ili bei ishuke.
Ещё видео!