#simbasportsclub #ClatousChama
SIO SIRI TENA! Ripoti za Kikachero Zaanika Ukweli Wote Chama Kushindwa Rs Berkane na Kurudi Simba
Klabu aliyekuwa anachezea mchezaji mwa Simba Mwamba wa Lusaka Claotus Chama Rs Berkane ya nchini Morocco imetaja sababu zilizopekea mchezaji huyo kurejea kwenye klabu yake hiyo ya zamani ambapo wao kama uongozi walijitahidi kufanya jitihada za kuhakikisha mchezaji huyo anabaki kwenye kikosi hicho.
Katika sababu hizo zinatajwa kuwa matatizo ya kifamilia ambapo kama utakumbuka mchezaji huyo mwaka mmoja uliopita aliondokewa na mke wake na hivyo kubaki na jukumu la kuwalea watoto na imeelezwa kuwa Chama anataka kuwa na familia yake popote atakapokuwa lakini kutokana na mazingira ya Morocco kuwa mageni kwake ilikuwa vigumu kwa upande wake kuishi na familia yake.
Lakini pia kushindwa kuendana na Ligi ya Morocco kwa haraka kumetajwa
na uongozi wa Berkane kama sababu nyinginye huku ikielezea kuwa hali ya hewa imechangia kwa kiasi kikubwa kwa Mwamba wa Lusaka kushindwa kwenda sawa na wenzake kwa haraka.
Kadhalika ‘lifestyle’ ya Morocco kuanzia vyakula, namna wanavyoishi na utamaduni wao na mambo mengine mengi n kikwazo kwa mchezaji huyo kushndwa kuendelea kuitumikia klabu hiyo.
Tayari mchezaji huyo ameshatambulishwa na uongozi wa Simba kuwa amerejea kwenye klabu yake hiyo baada ya kufikia makubaliano na Rs Berkane ya kuvunja mkataba kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Japo watu wamekuwa na maoni tofauti kufuatia kurudi kwake, wapo ambao wanasema kurudi kwake ni sawa na mwanafunzi aliyerudia darasa huku wengine wakimsifu na kusema nyumbani ni nyumbani, na mrudi kwao sio mtumwa.
Ещё видео!