ROSARI YA MACHUNGU SABA YA BIKIRA MARIA
Kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina
Sala ya kwanza
Ee Mungu wangu, nakutolea Rosali hii ya machungu saba ya Bikira Maria kwa ajili ya utukufu wako na kwa heshima ya mama yako Mtakatifu sana. Nitawaza na kushikania naye katika haya aliyopata. Nawe Maria Mama yetu nakuomba, kwa heshima ya machozi uliyomwaga wakati ulipopatwa na machungu haya, utujalie kutubu dhambi zetu. Amina.
Salamu Maria X 3
Ee Bikira Maria, Mama mwenye huruma, tukumbushe kila wakati mateso ya Yesu Kristo mwanao.
UCHUNGU WA KWANZA (LK 2:25-35)
Katika uchungu wa kwanza tunakumbuka wakati mzee mtakatifu Simeoni alipomtabiria Maria kwamba upanga wa uchungu utaufuma moyo wake, akimaanisha mateso na kufa kwake Yesu Kristo mwanae.
Tuombe neema ya kuvumilia mateso.
Baba Yetu x 1
Salamu Maria x 7
Atukuzwe Baba,
Ee Bikira Maria, Mama mwenye huruma, tukumbushe kila wakati mateso ya Yesu Kristo mwanao.
UCHUNGU WA PILI (MT 2:12-18)
Katika uchungu wa pili tunakumbuka wakati Maria alipolazimika kukimbilia Misri kwasababu Herode katili alitaka kumuua mtoto Yesu.
Tuombe neema ili miili yetu iwe kimbilio lake Yesu.
Baba Yetu x1
Salamu Maria x7
Atukuzwe Baba,
Ee Bikira Maria, Mama mwenye huruma, tukumbushe kila wakati mateso ya Yesu Kristo mwanao.
UCHUNGU WA TATU (LK 2:41-51)
Katika uchungu wa tatu tunakumbuka wakati Maria alipompotezs mwanae mpendwa na kwa siku tatu akamtafuta kwa uchungu mpevu na machozi.
Tuombe neema ya kudumu na Yesu mioyoni mwetu.
Baba Yetu x 1
Salamu Maria x7
Atukuzwe Baba
Ee Bikira Maria, Mama mwenye huruma, tukumbushe kila wakati mateso ya Yesu Kristo mwanao.
UCHUNGU WA NNE (LK 23:26-31)
Katika uchungu wa nne tunakumbuka wakati Maria alipokutana na mwanae wa pekee akiwa amebeba msalaba akielekea mlima Kalvari ambako alikua akienda kusulubiwa kwa ajili ya wokovu wetu.
Tuombe neema ya kudumu na Yesu siku zote.
Baba Yetu x1.
Salamu Maria, x7
Atukuzwe Baba,
Ee Bikira Maria, Mama mwenye huruma, tukumbushe kila wakati mateso ya Yesu Kristo mwanao.
UCHUNGU WA TANO (YOHN 19:25-27)
Katika uchungu wa tano tunakumbuka wakati Maria alipomwona mwanae Yesu ametundikwa juu ya msalaba na damu nyingi ikimwagika kutoka sehemu zote wa mwili wake.
Tuombe neema ya kufa mikononi mwa Yesu na Maria.
Baba Yetu x1
Salamu Maria, x7
Atukuzwe Baba,
Ee Bikira Maria, Mama mwenye huruma, tukumbushe kila wakati mateso ya Yesu Kristo mwanao.
UCHUNGU WA SITA (YHN 19:38-40)
Katika uchungu wa sita tunakumbuka wakati Maria alipomwona askari akimchoma mwanae ubavuni kwa mkuki na wakati mwili wa Yesu, baada ya kusgushwa msalabani, ulipolazwa mikononi mwake.
Tuombe neema ya kutotenda dhambi.
Baba Yetu x1
Salamu Maria, x7
Atukuzwe Baba,
Ee Bikira Maria, Mama mwenye huruma, tukumbushe kila wakati mateso ya Yesu Kristo mwanao.
UCHUNGU WA SABA (THN 19:40-41)
Katika uchungu wa saba tunakumbuka wakati Maria alipoona mwili wa mwanae wa pekee Yesu ukizikwa kaburini akitengana na mwanae ambaye kweli alimpenda mno.
Tuombe neema ya kitulizo kwa Mama Maria.
Baba Yetu x1.
Salamu Maria, x7
Atukuzwe Baba,
Ee Bikira Maria, Mama mwenye huruma, tukumbushe kila wakati mateso ya Yesu Kristo mwanao.
TUOMBE:
Ee Bwana Mungu wetu, kwa njia ya mateso na kifo cha Mwokozi wetu Yesu Kristu na kwa masumbuko yaliyompata mama yake Bikira Maria, ulileta wokovu kwetu sisi wakosefu. Twakuomba utujalie huu wokovu, tupate kuacha njia za dhambi na kupata yote mema aliyotuahidia Yesu Kristo yeye anayeishi na kutawala nawe na Roho Mtakatifu sasa na milele. Amina.
KUMBUKA
Kumbuka , Ee Bikira Maria, mwenye rehema, haijasikilika kamwe kwamba ulimwacha mtu aliyekimbilia ulinzi wako, akiomba msaada wako, akitaka umuombee. Nami kwa matumaini hayo ninakukimbilia ee Mama Bikira mkuu wa Mabikira, ninakuja kwako, ninasimama mbele yako nikilalamika mimi mkosefu, Ee Mama wa Neno la Mungu, usikatae Maneno yangu, bali uyasikilize kwa wema na unitimizie. Amina.
Ещё видео!