WAZIRI wa Ujenzi, Abdallah Ulega ametoa miezi mitatu kwa mkandarasi wa barabara ya Msongola -Mbande kukamilisha barabara hiyo kwa viwango kabla ya kuanza mvua ya masika.
Mkandarasi wa barabara hiyo ni Jonec (T) Ltd na JV Serc Construction ambaye anajenga barabara yenye urefu wa kilometa 3.8 na gharama zake ni Sh bilioni 5.4.
Akizungumza na wananchi wa Kata ya Msongola, Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, Ulega amesema barabara hiyo inapaswa kukamilika kabla ya mvua za masika na wananchi waanze kuona matunda ya kodi zao.
Amesema mkandarasi hadai fedha yoyote na badala yake wao ndio wanadai kazi hiyo hivyo, afanye kazi usiku na mchana kuhakikisha kabla ya mvua za masika, inakamilika.
Pia amemtaka kuzingatia ubora na viwango vya barabara hiyo ili isiharibike ndani ya muda mfupi.
Moja wa wananchi wa eneo hilo, Mussa Mfaume amesema kuwa barabara hiyo ni kilimo Cha muda mrefu kwa wakazi wa Msongola na kwamba mkandarasi anapaswa kujibu ni lini atakamilisha ujenzi huo.
Amesema kuwa mkandarasi ameanza kumwaga kifusi jana asubuhi na usiku na kwamba wanawasiwasi na ubora wa barabara hiyo.
"Barabara hii ndani ya mwaka mmoja tayari ina mashimo, hatuna imani na mkandarasi," amesema.
Ещё видео!