Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania, TRC, Masanja Kungu Kadogosa amekanusha taarifa za vyombo vya habari kwamba shirika hilo linao mpango wa kununua vichwa vya treni vinavyotumia mafuta ya Dizeli. Kwenye mahojiano na DW, Kadogosa amesema badala yake uko mpango wa kununua vichwa vichache vinavyotumia teknolojia ya umeme na mafuta kwa pamoja kukabiliana na adha ya hujuma dhidi ya miundombinu ya reli na hitilafu ya umeme.
Mapema gazeti la Citizen nchini humo liliripoti lilimnukuu Kadogosa akisema TRC inao mpango wa kununua vichwa vitavyotumia dizeli kwenye njia mpya ya reli iliyojengwa kutumia umeme. Msikilize Kadogosa na utoe maoni yako.
Ещё видео!