Tunapozindua kufungua mwaka wa Jubilei ya Shirika tangu Shirika lifike Tanzania, tunapenda kutazama wakati uliopita kwa shukrani kubwa, kuishi wakati wa sasa kwa mapendo makubwa na kutazama wakati ujao kwa matumaini thabiti, tukiongozwa na kauli mbiu yetu hii “kuishi kwa umoja na upendo’’. Masista wa kwanza wa SMI walifika Tanzania tarehe 26 Desemba 1972. Yaani!
Na Sr. Maria Agnes Mwanajimba, SMI, - Dar Es Salaam, Tanzania.
Shirika la Maria Imakulata lilianzishwa mnamo mwaka 1854 huko Wroclaw, nchini Poland, na Mtumishi wa Mungu Padre Johanne Schneider. Shirika lilisajiliwa na kupata hati ya Kipapa tarehe 22 Desemba 1897. Lilithibitishwa na hatimaye kupewa Hati ya Sifa. Mtumishi wa Mungu Padre Yohanne Schneider, Mwanzilishi wa Shirika la Masista wa Maria Imakulata, SMI katika wosia wake alisema‘’ Mkitaka kunishukuru mtende matendo ya huruma kwa jina langu.’’ Baba Mtakatifu Francisko anasema, Jubilei ni kipindi cha kuyatafakari yaliyopita kwa moyo wa shukrani, kuyaishi ya sasa kwa moyo wa hamasa na kuyakumbatia ya mbeleni kwa moyo wa matumaini. Ni wakati muafaka wa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema na baraka anazowakirimia waja wake hata bila mastahili yao. Ni muda wa kuomba msamaha kwa mapungufu yote yaliyojitokeza katika maisha na utume, tayari kuomba tena neema na baraka ya kusonga mbele kwa imani na matumaini zaidi.Hivyo basi tunapoelekea uzinduzi wa Jubilei ya miaka 50 hapo tarehe 8 Desemba tangu kuanzishwa kwa Shirika letu hapa Tanzania, ni nafasi pekee kwetu Wanaimakulata ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa mema yote aliyomtendea kila mmoja wetu, Shirika na Kanisa katika ujumla wake.
Masista wamisionari wa kwanza watatu kutoka Jimbo la Wroclaw nchini Poland, walifika nchini Tanzania tarehe 26 Desemba1972 kufuatia mwaliko wa hayati Askofu Arnold Cotey, SDS wa Jimbo Katoliki la Nachingwea na kuwakaribisha kwa wakati ule katika kijiji cha Kilimarondo. Masista walipofika maisha yalikuwa ni magumu na hata upatikanaji wa vitu muhimu ilikuwa ni ngumu, hivyo walipata chakula na mahitaji muhimu kutoka nyumba kuu ya Shirika kwa ajili yao na jamii iliyowazunguka. Pia walipata changamoto ya lugha, hivyo mara walienda kusoma lugha ya Kiswahili kwenye Shule ya Lugha Makoko, Jimbo Katoliki la Musoma, Tanzania ili waweze kuwasiliana vyema na watu mahalia na hata waliweza kujifunza lugha ya Kindonde ambayo ni lugha ya wanakilimarondo ili kuweza kuendesha utume wao vizuri. Baada ya kukaa, kutafakari na kupanga na Paroko, wakafikia muafaka kwamba, Masista wajielekeze zaidi katika Katekesi, Semina na Mafundisho ya Kikristo ili kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa watu wa Mungu.
Jambo la msingi lilikuwa ni ushuhuda wa maisha ya pamoja kati yao na wananchi wa Kilimarondo. Waliwaandaa waamini kuweza kupokea Sakramenti za Kanisa pamoja na kuadhimisha vipindi mbalimbali vya Liturujia ya Kanisa kwa uelewa na ushiriki mkubwa zaidi. Ibada ya Misa Takatifu chanzo na kilele cha maisha ya Kanisa ilipewa kipaumbele cha kwanza. Juhudi za katekesi na ushuhuda wa maisha ya watawa hawa zilikuwa ni msingi wa watu wengi kumwongokea Mwenyezi Mungu. Masista waliwashirikisha pia waamini walei katika maisha na utume wa Kanisa. Hivyo basi asili ya kufaulu kwa Masista wetu wa kwanza kulitegemea bidii yao ya kujua maisha ya kimisionari katika juhudi walizofanya, kuungana na Kristu kati ya watu, kutembea katika nuru yake, na kuishi katika upendo kati yao wenyewe. Lengo ni kumsogeza Kristo kati ya watu. Hivyo maneno haya ya Baba mwanzilishi, ‘’Msimamo wa kiroho hasa katika kuhudumia na kujitoa bila kuchoka’’ yaliwaongoza na kuwaletea heri na baraka tele!
Tafadhali Subscribe, Like, Comment na Share tone hili la upendo kwa ndugu jamaa na marafiki.
Jumuika nasi katika mitandao mingine ya Kijamii:
Instagram: [ Ссылка ]
Facebook: [ Ссылка ]
Mawasiliano:
JUGO MEDIA,
Sokoine Drive, Posta
P. O. BOX 34014,
Dar es Salaam.
For Bookings and other Enquiries
Phone Number +255757560764/657790405
#jugomedia #kanisakatoliki #familiatakatifu #wawata #uwaka #viwawa #australia #unitedstates #canada #america
Ещё видео!