Zaburi 74:20
[20]Ulitafakari agano;
Maana mahali penye giza katika nchi
Pamejaa makao ya ukatili.
Anaongelea eneo(location) katika nchi(ardhi) ambapo mambo yanayotendeka hapo ni ya ukatili,kama mambo hayo yanatendeka ina maana wapo wanaoyatenda hayo na wanakaa juu ya nchi.
Uchawi upo,wachawi wapo..na hawa watu wanaweza kuwa mtaani kwako na usiwajue ila ukabaki unajua kuna vitendo vya uchawi vinavyotendeka mtaani kwako.Hawa watu hufanya kazi kwa kujificha sana na ndio maana mchawi anaweza kukuroga ukashindwa kutembea na asubuhi ndio akawa mtu wa kwanza kuja kukusaidia.
Wakati Mungu anamtuma Musa kwenda kuwatoa waisraeli Misri alimpa pia ishara za kufanya ili Farao aamini kuwa ni Mungu aliyemtuma,na mojawapo ya ishara hizo ni kuangusha fimbo na kugeuka nyoka.Baada ya Musa kwenda kwa Farao akafanya hivyo kama Mungu alivyomuagiza,lakini Farao naye akawaita wachawi na waganga wake nao wakaangusha fimbo zao chini na zikageuka kuwa nyoka.Maandiko yanasema kuwa nyoka wa Musa akawameza wale nyoka wote wa wachawi.Ndani ya nyoka mmoja Mungu aliweka uwezo wa kuwameza nyoka wengi.Ndani yako kuna uwezo ambao Mungu ameuweka,ukiuangalia unaweza ukajiona kuwa una uwezo mdogo bila kujua kuwa kwa uwezo huo unaweza kutenda mambo makubwa sana kuliko fahamu za wanadamu zinavyofikiri.
UNAWEZA WASILIANA NASI AU KUTUMA SADAKA YAKO KWA NAMBA HII : 0657 173 322
Unaweza kutufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii
Like our Facebook: [ Ссылка ]...
Follow our Instagram: [ Ссылка ]...
Subscribe our YouTube: [ Ссылка ]...
Also Subscribe Roc worshippers youtube channel:[ Ссылка ]
and Subscribe Pastor Sunbella Kyando YouTube
[ Ссылка ]
Ещё видео!